Binadamu ni kiumbe anayependa kukubalika. Pengine, hata zaidi ya anavyojikubali mwenyewe.Iwapo mwanadamu anahisi kutokukubalika katika jamii inayomzunguka, huwa mpweke,mnyonge na mwenye msongo wa mawazo. Hisia ya kutaka kukubalika humfanya binadamu afanye lolote hata ikibidi kubadilisha muonekano wake ilimradi akubalike katika jamii inayomzunguka.Hali hii inaonyesha wazi kwamba mazingira yetu yana nguvu kubwa katika kuchangia fikra, matendo na imani zinazobobea katika tamaduni zetu. Faida za hisia hizi ni kwamba, zikiambatana na utashi mzuri, ufahamu binafsi na upeo, huleta mafanikio makubwa kwa mtu na kwa jamii .Hasara za hisia hizi ni pale zinapoambatana na ukosefu wa ufahamu binafsi, mwongozo potofu na upeo duni, kwani huwa ni chanzo cha majanga yanayotuongezea uduni wa maisha. Baadhi ya mitazamo duni inayotuathiri ilisababishwa na ukoloni uliotufunza chuki binafsi na kutuacha na pigo kubwa la fikra. Pigo hili limetuletea imani po...
Community Health Innitiaves