Skip to main content

Posts

HUDUMA YA AFYA KWA WATU WENYE ASILI YA BARA LA AFRIKA

African American Health  Program (AAHP) ni programu inayohusika na utoaji wa huduma za afya kwa jamii ya watu wenye asili ya bara la Afrika waishio kata ya Montgomery jimbo la Maryland. Jamii yenye afya ni mzizi wa taifa imara na lenye kuashiria uwezo mkubwa wa kushamiri katika nyanja mbalimbali. Lengo na dhumuni la programu ya AAHP ni kutoa huduma za afya zenye kukidhi mahitaji tofauti ya jamii husika ikizingatia lugha na tamaduni tofauti za jamii. Huduma hii isiyo na gharama kwako inalenga vipengele vifuatavyo; Saratani , Afya ya mama mjamzito na mtoto , Afya ya kinywa, Afya ya moyo, Magojwa ya zinaa na maambukizi, Ukimwi au HIV/ Aids na magojwa ya Kisukari, Usisite kuwasilina nasi kupitia African American Health Program 14015 New Hampshire Avenue Silver Spring, MD 20904 p:  240.777.1833 f:   301.421.5975 The African American Health Program is funded by the Montgomery County Department of Health and Human Services and administered by McFarland ...

VITUO VYA AFYA KWA WAKAZI WA KATA YA MONTGOMERY

  Mobile Med  ni huduma ya afya iliyo chini ya Montgomery Cares,  yenye kutoa huduma ya afya kwa wakazi wasio na bima ya afya . Huduma hii haitolewi kwa wale walio na visa za matembezi ya muda mfupi ( Hii ni kuepuka ugeni unaokuja nchini kwa nia ya kutumia mfumo bila kuchangia). Kuna imani kwamba, wale walio na visa zilizopitiliza muda wake, kwa namna moja au nyingine wanafanya kazi japo kinyume cha sheria na mapato yao huchangia mfumo kwa ujumla.   Huduma hii hutolewa kwa zamu na madaktari mbalimbali kutoka mahospitali makubwa kwa bei ndogo na yenye kuendana na kipato.  Mabingwa hawa ni wa magojwa mbalimbali na pia hutoa rufaa pale inapobidi kwa hospitali za   Shady Grove Adventist, Washington Adventist na   Suburban. Baadhi ya simu za vituo hivi ni (301) 493-2400, (301) 493-2400 Pitia www.mobilemedicalcare.org  VITUO VYA MOBILE MED Aspen Hill Clinic (Van) St. Mary Magdalene Church 3820 Aspen Hill Rd Aspen Hill, MD ...

Gonjwa la Saratani Laendelea Kuwa Tishio Ulimwenguni.

     Thanks                                                    

CSI INAKULETEA MAFUNZO YA JUU YA TAALUMA YA UKUNGA TANZANIA.

Childbirth Survival International Tanzania  inakuleta mafunzo ya juu ya kuendeleza taaluma ya Ukunga ili kuboresha huduma kwa mama mjaa mzito, watoto wachanga na familia kwa ujumla. [  Respectful Maternity Care (RMC)].                         Wahi kujiandikisha kupitia   Stella Mpanda  +255 754 432 584

The 2016 Susan G.Komen Race for Cure, Washington Dc

MOJA YA MAJIPU YANAYOIKUMBA JAMII YETU.

Kutoshiriki na kujitolea  katika kuchangia  rasilimali kwa ajili ya matumizi yetu sote kwa ujumla ni  jipu linaloikuimba jamii yetu. Pengine labda ni tamaduni  au  binafsi hayajatusibu. Lakini, pale yatakapotukuta  sio tu  familia, ndugu, jamaa au marafiki bali jamii kwa ujumla huangaika kutafuta namna ya kupata huduma au  kukidhi garama za  tiba ambazo hazishikiki. Sio vibaya kwa jamii yako kuwa ya msaada, bali njia hiyo  haileti utatuzi endelevu. Tufahamu kwamba tuko katika  nchi iliyoendelea na yenye mifumo mbali mbali iliyodhihirika kutoa  utatuzi endelevu kwa  watu kama sisi na wengine wengi wasio na ndugu,rafiki au jamii inayowajali. Hivyo basi pale tunapoombwa kushiriki katika jitihada za kukusanya senti za kutusaidia kwa ujumla au HARAMBEE basi tufanye kama tunavyochangia harusi zetu, tukijitokeza  kwa wingi,  tena kwa vifijo na ngoma, Susan G.Komen hutoa msaada mkubwa tu hata kwa ndugu zetu wahitaji...