M aziwa ya mama husifika kwa virutubisho vya hali ya juu na vyenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya mtoto mchanga. Baadhi ya virutubisho hivyo ni pamoja na protini,wanga,mafuta na madini ambayo ni muhimu katika ukuwaji wa mtoto mchanga na uimarishaji wa mfumo wa ufahamu ( Felden & Eidenkman, 2003 ). Vile vile, maziwa ya mama humpatia mototo kinga asilia yenye kumwezesha kupambana na baadhi ya magojwa na maambukizi yakiwemo; Maambukizi ya sikio na mafua ya mara kwa mara Magojwa ya mfumo wa chakula yanayopelekea kuharisha, pamoja na magojwa sugu kama crohn’s, celiac na necrotizing enterocolitis ( Bhandari et al., 2003,..Morrow er al., 2004 ) Magojwa ya atopic kama eczema na asthma ambayo asilimia kubwa husababishwa na matatizo ya mzio (allergies) Hupunguza hatari za unene wa utotoni Hupunguza hatari za kifo cha ghafla kwa watoto wachanga SIDS (Sudden Infant Death Syndrome) Baadhi ya faida kwa mama anayenyonyesha ni pamoja na k ujenga mahusiano ya karibu y...