Ni uhalifu unaojumuisha gari lililo katika mwendo huku likimwaga risasi kwa raia. Uhalifu huu wa kinyama ni sugu katika baadhi ya maeneo, hasa kwa ndugu zetu wanaoshiriki katika Magenge ya vurugu au gangs. Mbaya zaidi, uhalifu huu hutokea ghafla na kuchukuwa maisha ya raia wasio na hatia. Leo nilinusurika maisha nikiwa katika eneo la 7th st. NW DC. Ilikuwa mida ya saa kumi jioni ambapo shambulizi la ghafla la risasi zilizolia kama kifaru zilimiminika kutoka kwa gari isiyojulikana. Raia walikimbia , wengine kujificha na hata kulala chini ili kuokoa maisha . Baada ya dakika chache, kikosi kikubwa cha Police na Emergency Response 911, kiwasili na kutoa huduma ya haraka kwa majeruhi. Taarifa ya baadaye ya Fox 5 News, iliripoti kuwa kijana wa umri wa miaka 23,Mathew Shlonsky ambaye alikuwa mpita njia alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini. Polisi wakiongea na ra...