Fimbo ya kutembelea yaweza tumika na wazee au mtu wa umri wowote mwenye uhitaji wa kuimarisha msingi kabla ya kupiga hatua ili kupunguza atari za kuanguka. Vilevile, fimbo husaidia kupunguza uzito unaotua katika viungo vya mwili kama magoti ,mgongo na hips. Uzito wa mwili huongeza mwelemeo na maumivu hasa kwa watu wenye arthritis, maumivu ya mgongo na maumivu mengine ya viungo. Fimbo hii huweza kukunjika na kukaa ndani ya mkoba Fimbo ya kutembelea hutakiwa kuwa na urefu wa kutosha ili kuepuka kuinama na kuumiza mgongo. Urefu sahihi ni ule unaofika eneo la kiuno kwa mtu anayeitumia Watu wenye tatizo la usawa (balance ) huitaji mwangaza wa kutosha ili kupunguza atari za kuanguka. Fimbo hii ina taa yenye mwangaza wa kutosha kuona unapokwenda Waweza pata fimbo ya kutembelea katika duka lolote la vifaa vya afya. Fimbo yenye taa huondoa kadhia za kubebana na tochi. Ni vyema mkono uwe huru kusaidia mtu...