Mwanaume hutambulika kama shujaa katika uso wa jamii. Hutegemewa kuonyesha ujasiri wakati wote na hata kuficha hisia za ndani ili asiwe pungufu katika jamii inayomzunguka. Ripoti ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Kiakili nchini Marekani 'NIMH', imedhihirisha kuwa wanaume wengi huficha hisia zao za ndani kitu ambacho ni tofauti kubwa na wanawake. Utafiti huo ulioanza 2003, umesema kuwa zaidi ya wanaume millioni sita hupata hisia sugu za huzuni au Depression kila mwaka. Depression ni hali ya hisia sugu za huzuni wenye uwezo wa kudhoofisha afya ya kisaikolojia unaombatana na dalili zifuatazo ; Msongo wa mawazo K ukata tamaa au kupoteza matumaini Ugumu wa kushiriki shughuli za kila siku kama usafi wa mwili,mavazi na mazingira, Ukosefu wa usingizi Hasira za ghafla Kutoshiriki mazungumzo au eneo lenye watu Kupoteza ladha ya chakula au ongezeko la mlo BAADHI YA DALILI ZA DEPRESSION KWA WAN...