Shinikizo la damu hujullikana kama ' Silent Killer' kwani ni wengi wenye tatizo hili na huishi nalo hata miaka paasipo kulitambua. Shinikizo la damu hutuweka katika hatari za kiharusi (stroke), mshituko na hata kushidwa kwa moyo (heart attack and/or heart failure), upofu wa macho, pamoja na kushindwa kwa figo ambayo kazi yake kubwa ni kuchuja uchafu mwilini. Ili kugundua tatizo la shinikizo la damu mapema, ni budi kupata kipimo na kujenga tabia ya kujichunguza mara kwa mara . Uchunguzi na ufumbuzi wa mapema husaidia kupunguza madhara yatokanayo na shinikizo la damu. Baadhi ya dalili chache pale tatizo hili linapozidia ni pamoja na; maumivu ya kichwa, kizunguzungu, kichefuchefu, uhafifu wa kuona, kupoteza uwezo wa kutambua na hata kuzimia. Shinikizo la damu uhashiria kishindo au kipondo cha mzunguko wa damu katika kuta za mishipa mwilini. Kipondo hicho kinapokuwa kikubwa kwa muda mrefu, hupeelekea kudhoofika kwa mishipa ya